Saturday, June 30, 2012

Mnyama Atabaki Kuwa Mnyama, hata kama akiwa na PhD: Utashi hakuna!


Mshipa Ugonjwa au Umwinyi: Unaathiri vipi pato la Taifa letu?


Tuesday, June 26, 2012

Vigogo waficha bilioni 300 Uswisi

 
Monday, 25 June 2012 21:43

Mwandishi Wetu
KITENGO cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kinachunguza Sh303.7 bilioni ambazo zinadaiwa kukutwa kwenye akaunti sita za Watanzania, wakiwamo wanasiasa, katika benki mbalimbali nchini Uswisi.
Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya Interpol kilichonukuliwa na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen, kimesema baadhi ya wanasiasa nchini na watu wengine ndiyo wanahusika na ufisadi huo kwa kuwa na akaunti zenye fedha nyingi nchini Uswisi.
Fedha hizo zimeelezwa ziliingizwa katika akaunti hizo na kampuni za uchimbaji mafuta na kampuni za uchimbaji madini, ambazo zinafanya kazi Tanzania.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti, zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa.

Kiasi hicho cha fedha kilichofichwa Uswisi, kinatosha kuendesha Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa miaka mitano, au kusaidia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kuendesha shughuli zake kwa miaka miwili.

Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi moja.

"Wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini," kilidokeza chanzo hicho.

Mabilioni hayo yamebainika kufichwa wakati takwimu zilizotolewa na Umoja wa Taasisi za Kupambana na Rushwa barani Afrika ikiwamo Tanzania, zikionyesha kwamba Sh22 trilioni, zimekuwa zikitoroshwa nchini humo na kufichwa katika nchi za kigeni, ikiwamo Uswisi.

Fedha hizo zimebainishwa na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB), iliyotolewa hivi karibuni, ikibainisha nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, na kiwango cha fedha zake zilizohifadhiwa huko.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hivi sasa inafuatilia suala hilo kwa mamlaka za Uswisi, ili kujua fedha hizo ziliko na nani anazimiliki.

Mbali ya Tanzania, nchi nyingine ambazo zina fedha nyingi katika benki za Uswisi ni Kenya (dola 857 milioni), Uganda (dola 159 milioni), Rwanda (dola 29.7 milioni) na Burundi dola 16.7 milioni.
Jumla ya fedha zilizoko katika benki za Uswisi kutoka nchi hizo nyingine za Afrika ni Faranga 1.53 trilioni za nchi hiyo na ripoti hiyo imeelezwa kuwa kuna msukumo wa kimataifa wa kuitaka nchi hiyo izitake benki zake, kubadilishana taarifa za wateja na serikali za kigeni.

Ripoti hiyo imekuja wakati pia Uswisi ikiwa na rekodi ya kuhifadhi mabilioni ya dola kutoka nchi za kigeni ikiwamo Afrika, kwani iliwahi pia kuhifadhi dola zaidi ya bilioni 1.5 za aliyekuwa Kiongozi wa Kijeshi wa Nigeria, Jenerali Sani Abacha na dikteta Mobutu Seseseko wa iliyokuwa Zaire.

Gavana azungumza
Akizungumzia ripoti hiyo, Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndulu (pichani) alisema uamuzi huo wa Uswisi wa kuanza kufungua milango utaiwezesha BoT kuwa na rekodi ya kiasi halali cha fedha zilizopo katika nchi hiyo.

Profesa Ndulu alifafanua kwamba katika siku za nyuma, Uswisi haikuwa imefungua milango kwa kutaja kiasi cha fedha za wateja wake walioweka fedha katika benki zake, hivyo ilikuwa vigumu kwa mamlaka za ndani kuweza kufanya uchunguzi.

"Ndiyo kwanza wameanza kufungua milango, sisi siku zote tulikuwa hatuwezi kujua nini kinaendelea. Lakini, angalau sasa tutaweza kujua na kuwa na rekodi baada ya uamuzi huo wa kufichua kiasi cha fedha kilichomo katika benki zake," alifafanua gavana.
Kiutaratibu, BoT inapaswa kuwa na rekodi ya fedha halali za Watanzania zilizopo nje ya nchi.

Kauli ya Takukuru
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alikaririwa na The Citizen hivi karibuni alisema kuwa ofisi yake ina taarifa kuhusu suala hilo na kwamba wanaanza mawasiliano na Serikali ya Uswisi kujua ukweli wake.

Dk Hoseah alisema taasisi hiyo inataka kujua jinsi gani fedha hizo ziliwekwa kwenye benki za Uswisi, watu waliohusika na namna uhamishaji wa fedha hizo ulivyofanyika.

"Tutakapogundua fedha hizo zimetoka wapi, tutafuata taratibu zinazohusika kuhakikisha zinarudi nchini," alisema Dk Hoseah na kuongeza: "Tutatumia sheria zilizopo katika nchi hizi."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa yuko likizo, hivyo aulizwe msemaji wa Jeshi la Polisi.
Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema hawajapata ripoti hiyo na kwamba atawaomba watu wa uchunguzi kumpatia, ili aweze kutoa taarifa.

Saturday, June 23, 2012

Madaktari na Siasa : Tanganyika 

Je unawatambua madaktari hawa na mchango wao kakika kugombea uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1948 - 1950:
  • Dr. Vedasto Kyaruzi
  • Dr Joseph Mutahangarwa
  • Dr Wlibard Mwanjisi
  • Dr Michael Lugazia
  • Dr Luciano Tsere 

Utajiri wa gesi wagunduliwa Mtwara, Lindi

 
Sunday, 17 June 2012 09:22

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Mussa Juma, Arusha.
KAMPUNI mbili za kimataifa, zimegundua futi trilioni 20.97 za ujazo za gesi asilia mashariki mwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kampuni hizo ni Statoil ya nchi Norway na Exxon ya Marekani.

Profesa Muhongo aliyasema hayo jana alipouwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, kufuatia kukamilika kwa utafiti wa gesi hiyo.

“Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwapo na kasi kubwa ya utafutaji wa mafuta na gesi asili hapa nchini. Utafiti huo ulijikita zaidi kwenye Bahari ya Hindi kwenye maji ya kina kirefu,kiasi cha gesi iliyogundulika katika kina cha maji marefu kinafikia takribani futi za ujazo trioni 20.97 ikijumuisha pia kisima kilichogunduliwa wiki hii cha Lavani,” alisema.

Alisema kampuni hizo zimegundua na kuthibitisha kuwapo kwa futi za ujazo 20.97 za gesi asilia katika kisima cha Lavana kilichoko kitalu namba mbili Mashariki mwa Lindi.

Alisema imebainika kuwa kisima kilichochimbwa Songosongo Kisiwani na kukamilika Mei mwaka huu, kina uwezo wa kuzalisha futi za ujazo milioni 60 za gesi kwa siku.Profesa Muhongo alisema pia imegungulika kwa katika visima nane vilivyochimbwa kwenye bahari ya kina kirefu, saba vina gesi asili.

Alisema hata hivyo kisima kimoja kinaendelea kuchimbwa kwenye kitalu namba tatu.Alisema kupatikana kwa gesi asilia ya kutosha kutaiwezesha Serikali kuwa na uhakika wa matumizi ya nishati hiyo na kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa.

“Baada ya miaka mitatu ijayo gesi asilia itaweza kutumiwa na Watanzania wengi ikiwani ni pamoja na watumiaji wa majumbani na hivyo kuepukana na matumizi ya mkaa na kuni,”alisema Profesa Muhongo.
Kugundulika kwa kesi katika maeneo hayo,pia kunatarajiwa kuongeza ajira kwa vijana.

Serikali yaahidi walioua mtalii kukamatwa

Saturday, 23 June 2012 10:01
0diggsdigg
Mussa Juma, Dodoma
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, wamemhakikishia Balozi wa Uholanzi nchini, Dk Ad Koekkoek, kuwa majangili wote waliohusika na mauaji ya mtalii Eric Brekelmans(53) wanakamatwa.

Hatua hiyo inafuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete, kuwaagiza mawaziri hao kufuatilia mauaji hayo, hali iliyosababisha kukatisha kuhudhuria vikao juzi kwenda Arusha kukutana na Balozi Koekkoek na mjane wa Brekelmans, Annelnes.

Kifo hicho kilitokea katika Kambi ya Moivaro,Kijiji cha Robanda, kwa kupigwa risasi na majangili.
Mawaziri hao, waliondoka kwa ndege ya Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) juzi mchana mjini Dodoma kwenda Serengeti kufuatilia tukio hilo.

Pia, majangili hao walimuua Meneja msaidizi wa kambi hiyo, Renatus Bernard na watalii wengine 40 waliporwa mali zenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni.

Wakizungumza juzi usiku mjini Arusha na balozi huyo na mjane nyumbani kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Leopard, Zuher Fazal,mawaziri hao walitoa pole kwa tukio hilo ambalo walisema siyo la kawaida na ndiyo maana walitumwa na Rais Kikwetekwenda eneo la tukio.

Balozi Kagasheki alisema,tukio hilo limeisononesha Serikali na Watanzania kwa ujumla, kwani dunia nzima inatambua amani na utulivu uliopo nchini.

Dk Nchimbi alisemaSerikali itahakikisha wote waliohusika na mauaji hayo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.

Naye mjane Brekelmans, Annelnes aliishukuru Serikali ya Tanzania, kwa ukaribu ilioonyesha na kwamba, mumewe aliuawa kwa kupigwa risasi kifuasi wakati akipambana na majangili hayo, huku yeye akijeruhiwa kwa panga.

Hata hivyo, Annelnes alisema usalama katika kambi hiyosiyo mzuri, kwani ina eneo kubwa na hakuna usalama wa kutosha, jambo ambalo alishauri lirekebishwe.

Kwa upande wake,Balozi Dk Koekkoek alieleza kusikitishwa na tukio hilo, huku akimshukuru Rais Kikwete, mawaziri hao na watu wengine ambao wamekuwa wakishirikiana naye tangu tukio hilo kutokea.
Black Mamba Vs Taifa Stars (matuta yatuangua) 

Sunday, June 17, 2012

Shivji asisitiza umakini uwekezaji wa ardhi Send to a friend
Saturday, 16 June 2012 08:53
0diggsdigg
Profesa Issa Shivji
Kelvin Matandiko
MWENYEKITI wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Profesa Issa Shivji amesema,Tume ya kuratibu maoni ya Katiba Mpya ikumbuke kujadili umakini wa suala la nchi za Magharibi kuwekeza katika ardhi kwa ajili ya kambi za kijeshi.

Profesa Shivji alisema hayo kupitia mhadhara wake wa katiba unaorushwa na kituo cha ITV jijini Dar es Salaam na kwamba nchi nyingi barani Afrika ambazo zilifanya hivyo zimejikuta kwenye machafuko ya vita.

“Ni lazima Tume wakumbuke jambo hili muhimu sana, nchi za kibepari wana mikakati ya kuweka kambi zao za kijeshi barani Afrika,ukitoa eneo la ardhi kwa wawekezaji wa aina hii watavuruga nchi”, alisema na kuongeza:

Ni marufuku kutoa eneo la ardhi,anga na maji kwa ajili ya kambi ya kivita,ni muhimu kujua hilo ili kuinusuru nchi”, alisema Shivji.

Akitoa mfano wa Mataifa ambayo yameathirika kwa sababu ya kutoa sehemu ya ardhi ndani ya nchi zao ni pamoja na Iraq,Somalia na Pakstan na sehemu nyingine barani Afrika.

Alisema, hali hiyo inaweza kusababisha kuuza uhuru wa watu. Profesa Shivji akatoa mfano wa kitabu kilichoandikwa na Edward Sokoine mwaka 1982 kinachozungumzia Taifa kuuza uhuru wake ili kupata misaada kutoka nje.

“Nchi za kiafrika zinasumbuliwa na tatizo la kiuchumi hivyo inatoa eneo la ardhi kwa uwekezaji ili kupata misaada ya kifedha,tumeona madhara mengi yaliyoanza kujitokeza,”alisema.

Saturday, June 16, 2012

Budget draws mixed reaction

.Some fault reliance on same revenue sources
.LOthers praise it as balanced in tackling crisis
Finance minister, Dr William Mgimwa displays briefcase containing the 2012/2013 Budget Speech as he heads for Parliament ready to table it.
The public and members of parliament yesterday challenged
the government to look for alternative sources of revenue instead of relying on the traditional sources.
Reacting in interviews immediately after Finance minister Dr William Mgimwa tabled his budget proposals, some members of parliament said the budget has increased but the government has not outlined strategic plans to control expenditure.
Leader of Opposition in the Parliament Freeman Mbowe said the government has traditionally increased taxes on soft drinks, beers, spirits and cigarette and wine instead of looking beyond these into other sources of income.
He cited construction industry saying that it could be one of the important sources of government revenue.
Mbowe also challenged the government to control expenditure, saying it had not shown enough commitment to do so, through cutting down unnecessary allowances as stated in the national development plan.
He said the budget also lacked plans to support farmers who constitute 75 percent of the country’s population.
Mbowe who is the Hai MP said the government has outlined plans to curb inflation such as establishing sugar plantations and factories as well as providing permits for importing sugar, but it does not state how this will help to reduce inflation.
Kigoma–South MP David Kafulila (NCCR-Mageuzi) said the budget has been focused on expenditure rather than development.
He said out of the 15trn/- set for the budget for the financial year 2012/2013 only 4trn/- has been set aside for development.
“This shows that there is no hope for future development. The government should also outline measures to curb overexpenditure,” Kafulila said.
He proposed to cut down expenditure on official trips abroad by allowing only the President, Speaker and Chief Justice to use business class.
Bariadi –West MP John Cheyo said there were still challenges in harmonising revenue and expenditure in the budget.
“The government spends too much while it collects very little,” Cheyo said.
He also said that the country was still dependent on external support in development budget, noting that the system will continue to affect development activities in the country.
Cheyo also challenged the government to look for other sources of revenue.
Wolfgang Solzbacher whois director of kfw Bank of Germany said the budget figures are very high but the actual money spent for development programme is meagre
He said the budget of this year is better than last year’s which was too ambitious.
The outspoken Kigoma North Legislator Kabwe Zitto, said it is a budget which will benefit people living in urban areas.
He pointed out that the budget has provided relief for the use of natural gas for home cooking which is mostly used by urban dwellers.
However he commended the government for introducing excise duty on music and film products saying the move would improve the lives of local artists.
On the national debt, Zitto said the government has to make sure it uses effectively all the money borrowed.
He said the government should channel more money into development plans and cut unnecessary spending.
For his part, Mpendae Member of parliament (CCM) Salim Turky praised the budget as generally good for cutting across all issues.
However he said the government was not supposed to increase tax on soft drinks. He proposed a heavy taxing of beer and spirits.
He urged the government to use the foreign aid more effectively which would fast track development.
The Chairman of Civic United Front (CUF ) Prof Ibrahim Lipumba, said the government has failed to meet its commitment in agriculture.
He said in the year 2010 the government set aside 3 percent of the budget for agriculture while last year only 1.6 percent was allocated.
“Tanzania including many African countries have already committed to increase their budget in agriculture to ten percent. With this trend we cannot alleviate poverty, Prof Lipumba said, adding: “Since 50 percent of costs go to food and there is need to support agriculture to improve livelihood of Tanzanians.”
He also urged the government to cut expenses and put the money into development projects.
“Recurrent budget has been increasing anually. This is not healthy for the development of this nation. We have to make sure it come down,” he concluded.

SOURCE: THE GUARDIAN